JOSE CHAMILION AWAPIGIA DEBE RADIO & WISLE

Baada ya kufunika vilivyo kwa kutoa burudani ya nguvu katika tamasha kubwa ambalo limefika huko nchini Uganda hivi karibuni msanii Jose Chameleone amesema kuwa amewaomba mashabiki na wadau kuwapa sapoti wasanii wa Goodlyfe, Moses Radio na Weasel TV.
Chameleone ambaye ni ndugu na Weasel TV alitumia nafasi hiyo ya
kuwaomba mashabiki katika tamasha hilo kutokana na kwamba wasanii hao
wamekuwa ni wenye mafanikio makubwa na kwamba katika wiki mbili zijazo
wanatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao waliyoibatiza jina ‘Obudde’.
Aidha Jose Chameleone alionyesha kuwa yeye ni gwiji na mwenye kipaji
katika tamasha lake la ‘Badilisha’ haswa alipoweza kuimba zaidi ya
nyimbo 40 ambapo pia aliziimba nyimbo za wasanii mbalimbali Afrika
Mashariki kama wimbo wa Kigeugeu wa Jaguar, Mukama wa Judith Babirye,
Bread and Butter kutoka kwao Moses Radio na Weasel TV, Kasepiki wa Bebe
Cool na Wendi wa Bobi Wine.
No comments