WEMA AMPULIZIA MBWA WAKE PAFYUMU YA DOLA 120
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu kama kawa ameshuka na mpya ya kumpulizia mbwa wake pafyumu yenye thamani ya dola 120 (zaidi ya shilingi 180,000).Mkali huyo asiyekaukiwa na matukio Bongo amefunguka kuwa analazimika kumgharamia mbwa huyo pafyumu hiyo kwani ni moja kati ya viumbe ambavyo anavihusudu kupita maelezo.
“Lazima anukie kama mimi ninavyonukia, pafyumu humfanya anukie vizuri hata ninapokuwa nimetoka naye mitaani naye anaonekana kweli ni mbwa wa staa,” alisema Wema.Kuhusu manunuzi, mkali huyo anayekimbiza kwenye soko la filamu Bongo alisema mara nyingi pafyumu hizo huwa anaagiza kutoka nje au kwa watu wake maalum hapa Bongo ili kuwa na utofauti wa ubora na wengine…
WEMA AMPULIZIA MBWA WAKE PAFYUMU YA DOLA 120
Reviewed by bongohitz1
on
3:07:00 PM
Rating: 5
Reviewed by bongohitz1
on
3:07:00 PM
Rating: 5

No comments