MATONYA ALIZWA SHILLINGI MILLIONI SITA NA BONGO MOVIE"Mwenyewe akili na kusema tasnia ya bongo movie ina mapepo na inahitaji msaada wa kiroho zaidi ili ipate upako na kuombewa"
Mwandishi wetu alimtafuta Tonya Boy na kuzungumza naye juu ya ishu hiyo kuwa kulikoni hadi alilizwa kiasi hicho cha pesa, ndipo alipodai kuwa kuna mmoja wa mademu wazuri wanaovuma kwenye tasnia bongo movie ndiye aliyefanya mchezo huo mchafu kwani alijifanya anampenda sana kumbe alikuwa anamuigizia na alikuwa na ishu yake.
Alidai kuwa baada ya tukio hilo kutokeo demu huyo hakumuona tena na alikuja kusikia yupo mkoani kitu ambacho kilimfanya aishiwe nguvu kwani hakuamini kilichotokea na hapo ndipo alipoamini kuwa mademu wa tasnia hiyo ni wapigaji na ukiwaonesha kwako utajuta.
“Bongo movie hakuna demu yani hata bure siwataki tena yani wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi dah kweli hii tasnia ina laana na inahitaji kuombewa kwani wasanii wake wanatamaa ya hela na wanamapepo ya ngono yani wakimuona mwanaume ana hela basi mate yanawatoka, hata wa bure siwataki tena,” alidai.
Hata hivyo alipoulizwa jina la msanii huyo wa filamu alishindwa kumtaja kwa madai kuwa hata kama aliiba kiasi hicho cha pesa lakini kwa upande wake hana bifu naye ingawa hatamani hata kumuona.
Lakini kwa jisi tunavyojua huyu jamaa amefunga pingu za maisha na mwanadada wa kiislamu katika ndoa ya kiislam na hata hivyo walibarikiwa mtoto katika maisha yao ya ndoa, iweje atoke nje ya ndoa? Hii ni hali ya usaliti na kutoheshimiana katika mapenzi ya dhati. Mwandishi wetu hakusita kuweka picha za harusi za msanii huyo
Matonya akiwa na Mke wake pamoja na msanii mwenzake Banana Zorro
Hapa akipeana mikono na mtu mzima Prof.Jay
No comments