MOYO WA FLAVIANA MATATA KWENYE KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA.

Mwanamitindo mtanzania Flaviana
Matata ametoa life Jackets mia tano (500) na kuzikabidhi kwa mamlaka ya
bandari Mwanza (TPA) kama kumbukumbu ya miaka kumi na sita ya ajali ya
meli ya MV BUKOBA.
Flaviana amesema “nimetoa hizo
life Jackets kwa ziwa Victoria ambapo ajali hiyo ndipo ilipotokea ambapo
mama yangu alikua mmoja wa waliofariki dunia”
Flaviana Matata mwenye makazi
yake London U.K na New York Marekani anakofanya kazi, amesema alitoka na
hizo Life Jackets nje ya nchi baada ya kuzioda kiwandani na angependa
watanzania wenye uwezo wa kufanya hivyo wafanye pia, yeye ameshafungua
milango”
No comments