Ishu ya mtangazaji maarufu wa kituo cha televisheni cha TV1 Ezden Jumanne kurekodiwa video ya utupu na kupostiwa mtandaoni bila ridhaa yake kitendo kilichofanywa na aliyekuwa mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Moza imefikia patamu baada ya demu huyo kutupwa selo huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Inasemekana demu aliamua kuvujisha video hiyo baada ya kutibuana na mshikaji mpaka kufikia hatua ya kuachana.Kwa mujibu wa Ezden uvujishwaji wa video hiyo ulikuwa na lengo la kumdhalilisha na kumvunjia heshima katika jamii hivyo hana la kufanya zaidi ya kuripoti tukio zima poilisi ili sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
|
Ezden(kulia) na Moza(kushoto) |
Matukio ya wapenzi kusambaza picha na video za utupu za wenzi wao yamekuwa yakishika kasi moja ya sababu ikiwa ni wivu wa kimapenzi baada ya wapenzi kuachana pamoja na ulimbukeni na ushamba uliopitiliza.Mara nyingi sana matukio kama haya wamekuwa wakifanyiwa akina dada lakini hakuna hata mmoja aliyechukua hatua stahiki ili sheria ichukue mkondo wake zaidi ya kuendelea kudhalilika mtaani.
No comments