Sevilla bingwa wa UEFA mtoto 2014
Klabu ya Sevilla ya nchini Hispania usiku wa kumakia hii leo ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya barani Ulaya *Europa League* baada ya kuwabanjua Sporting Lisboa Benfica, katika mchezo wa hatua ya fainali ambao ulipigwa katika uwanja wa Juventus huko mjini Turin nchini Italia.
Sevilla ambao walionekana kuwa makini katika safu ya ulinzi wakati wote, iliwalazimu kusubiri hadi katika muda wa mikwaju ya penati baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana ndani ya muda wa dakika 120.
Katika hatua ya mikwaju ya Penati Sevilla walifanikiwa kupata mikwaju minne huku Benfica wakipata mikwaju miwili.
Hii inakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Benfica kuukosa ubingwa wa Europa league kwenye hatua ya mchezo wa fainali, ambapo kama itakumbukwa vyema msimu uliopita walikubali kufungwa mabao mawili kwa moja na Chelsea kutoka nchini Uingereza.
No comments