Safari ya kuelekea Brazil kwenye fainali za kombe la dunia, tuangalie timu ya Australia
Timu ya taifa ya Australi ilifanikiwa kutinga katika fainali za kombe la dunia za mwaka huu zitakazocheza nchini Brazil, ikitokea ukanda wa barani Asia ambapo ndipo iliposajiliwa, lakini kijografia ipo katika ukanda wa Oceania.
Ikicheza katika ukanda wa barani Asia Australia ilifanikiwa kuwa miongoni mwa mataifa kumi yaliyoingia kwenye hatua ya mwisho ambayo ilihusisha makundi mawili yaani A na B.
Ikitokea katika kundi B, Australia ilifuzu moja kwa moja baada ya kuwa moja ya nchi mbili ambazo zilitakiwa kufuzu kutoka katika kila kundi ikitanguliwa na Japan ambayo ilikuwa ikiongoza kundi la pili.
Katika historia ya ushiriki wa fainali za kombe la dunia.
Nchi ya Australia itakua ikishiriki faianli za kombe la dunia za mwaka huu kwa mara ya nne, baada ya kufanya hivyo katika misimu mitatu tofauti iliyopita.
Katika historia ya ushiriki wa fainali za kombe la dunia.
Nchi ya Australia itakua ikishiriki faianli za kombe la dunia za mwaka huu kwa mara ya nne, baada ya kufanya hivyo katika misimu mitatu tofauti iliyopita.
Kwa mara ya kwanza Australia walifuzu kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 1974 zilizochezwa Ujerumani Magharibi, kisha wakarejea tena kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2006 zilizochezwa nchini Ujerumani na katika fainali za mwaka 2010 na pia nchi hiyo ilikua miongoni mwa nchi shiriki zilizokwenda Afrika kusini.
Mafanikio makubwa katika ushiriki: Hatua ya mtoano
Viwango vya ubora wa soka duniani: 59
Mchezaji muhimu
Tim Cahill anatazamwa kama mchezaji muhimu katika kikosi cha timu ya taifa ya Australia kwa mwaka huu.
Kocha: Ange Postecoglou (Ugiriki)
Jina la timu ya taifa: Socceroos
Wachezaji waliowahi kutamba wakiwa na timu ya taifa ya Australia miaka ya nyuma: Johnny Warren, Mark Viduka, Scott Chipperfield
Katika fainali za mwaka 2014 timu ya taifa ya Australia imepangwa katika kundi la pili lenye timu za Hispania, Uholanzi pamoja na Chile.
Australia wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa dunia mwaka huu kwa kucheza na timu ya taifa ya;
Arena Fonte Nova, Salvador
13 June 2014
Chile Match 4 Australia
Arena Pantanal, Cuiabá
18 June 2014
Australia Match 20 Netherlands
Estádio do Maracanã, Rio de Janeiro
23 June 2014
Australia Match 35 Spain
No comments