Exclusive Video: Umeiskia hii kuhusu Wenger aliivyokiri kuwa safu yake ya ushambuliaji ni butu.......Tazama Video
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, amekiri safu yake ya ushambuliaji ilikua kikwazo kikubwa katika harakati za kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Arsene Wenger, amekiri suala hilo kwa mara ya kwanza baada ya kupingana na vyombo vya habari kwa kipindi kirefu, ambavyo vilikuwa vikiikosoa safu yake ya ushambuliaji ambayo inongozwa na Olivier Giroud.
Wenger, amesema endapo safu yake ya ushambuliaji ingekua na makali kama ilivyo kwa Liverpool pamoja na Man City, hii leo angekua anazungumza maneno tofauti mbele ya waandishi wa habari.
Mzee huyo kutoka nchini Ufaransa pia akazungumzia ubutu wa safu yake ya ushambuliaji ambao, unakifanya kikosi chake kumaliza katika nafasi ya nne, kwani hata kama ikitokea Chelsea inapoteza mchezo wake wa mwishoni wa msimu huu na wao wakashinda wao dhdii ya Norwich City bado nafasi ya nne itakuwa inawahusu kutokana na utofauti wa mabao.
No comments