Robin Van Persie akanusha kuondoka Man Utd
Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Robin van Persie amekanusha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari mwanzoni mwa juma hili kwa madai yu njiani kuondoka kwenye klabu ya Man Utd baadaya kuchoshwa na mwenendo wa klabu hiyo.
Robin van Persie amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na pia anaamini vyombo vya habari vinataka kumtengenezea mazingira mabaya kati yake na mashabiki wa klabu ya Man Utd pamoja na viongozi wa klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo mwenye 30 amesema siku ziote amekua mkimywa klabuni hapo na hakuwahi kuzungumza na chombo chochote cha habari juu ya taarifa za kutaka kuondoka hivyo ameshangazwa na suala hilo kupewa kipaumbele.
Hata hivyo mkataba wa Robin van Persie na klabu ya Man Utd unatarajia kufikia kikomo mwaka 2016.
No comments