Recent comments

Breaking News

Lupita Nyong'o alipamba jarida la Hollywood Reporter, tetesi za kuwa mpenzi wa rapper K'Naan zachukua sura mpya.

Lupita Nyong
Muigizaji wa kike toka Kenya, Lupita Nyong’o ameendelea kuwa taswira ya mauzo inayosaidia kusapoti biashara nyingi kubwa.
Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar amepewa nafasi ya kulipamba jarida maarufu la Hollywood Reporter akiwa amepoz na waigizaji wenzake wa kike, Michelle Dockery na Micaela Erlanger.
Kwa upande mwingine, tetesi za Lupita Nyong’o kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapper Msomalia, K’naan zinaendelea kuchukua sura mpya ambapo chanzo kimoja kimeliambia Us Weekly kuwa wawili hao wamekuwa na uhusiano kwa kificho tangu miezi sita iliyopita na kwamba wanataka mambo yaende taratibu.
K’naan ana watoto wawili wa kiume aliowapata na mkewe wa zamani Deqa Warsame na imedaiwa kuwa Lupita Nyong’o hajawaona watoto wa rapper huyo.

No comments