Keyshia Cole aeleza sababu za kuachana na mume wake kwenye wimbo wake mpya 'Next Time', usikilize hapa
Mwimbaji wa R&B, Keyshia Cole ambaye alikuwa akikwepa maswali ya waandishi wa habari kuhusu sababu za kuachana na mme wake Daniel Gibson, ameamua kuziweka sababu hizo zote kwenye wimbo wake mpya uliotoka jana unaoitwa ‘Next Time’.
Katika wimbo huo mwimbaji huyo ameonesha kuwa usaliti ndio chanzo kikubwa cha kushindwa kumvumilia Daniel Gibson.
Haijafahamika moja kwa moja kwa moja kama kila alichoimba ni ukweli wa ndoa yake ama kuna usanii pia umeongezwa.
Keyshia anaimba akiuliza kuwa kama kweli jamaa alikuwa anampenda kwa nini alimleta mwanamke mwingine kwenye nyumba yake, sehemu ambayo mwanae alilala.
“Kwa maana...ni kuhusu kuwa katika uhusiano, kuwa na uzoefu wa maumivu ya uhusiano na kutotaka kurudi huko tena.” Amesema Keyshia wakati anaeleza maana ya wimbo huo kwenye mahojiano aliyofanya na The Breakfast Club.
“Na pia ni kuhusu kuutoa moyo wako na kuruhusu mtu awe na uwezo wa kuwa karibu na wewe ambapo wanaweza kukuumiza.” Aliongeza.
No comments