Recent comments

Breaking News

Jason Robert atangaza kujiweka kando na soka.

 Jason Robert atangaza kujiweka kando na soka
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu za Wigan na Blackburn Rovers, Jason Roberts ametangaza kustahafu soka kufuatia jeraha la paja ambalo linamsumbua tangu mwezi disemba mwaka 2012.
Wigan Jason Roberts ametangaza kustahafu soka, akiwa na klabu ya Reading inayoshgiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza kwa kusema ameamua kufanya hivyo baada ya kushauriwa na familia yake ambayo imekua ikimuuguza kwa kipindi kirefu.
Jason Roberts ambae alikua miongoni mwa wachezaji walioipandisha daraja Wigan na kucheza ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwaka 2004 amesema anatambau amefanya maamuzi magumu, lakini hana budi kuamua hivyo kutokana na hali yake kiafya.
Amesema kabla ya kutangaza maamuzi ya kustahafu soka, alikua akisita kufanya hivyo kutokana na kuhofia huenda mashabiki wake wangejisikia vibaya, kutokana na ukaribu uliopo, lakini alikaza moyo na kutangaza mwisho wa safari yake ya kucheza soka ambayo ilianza mwaka 1995 akiwa na klabu ya Hayes ya nchini kwao Uingereza.
Hata hivyo Jason Roberts, ambae kwa bahati mbaya alishindwa kuisaidia Blackburn Robvers isishuke daraja kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza hadi ligi daraja la kwanza katika msimu wa mwaka 2011-12, amemshukuru kila mmoja ambae alikua akimuwezesha kucheza soka na kufunga mabao, kwa kusema daima atawakumbuka na kuwaheshimu.
Kama itakumbukwa vyema Roberts, mwenye umri wa miaka 36, alifunga bao lake la mwisho katika ligi ya nchini Uingereza akiwa na klabu ya Reading wakati wa mchezo dhidi ya Southampton ambao walikubali kulala kwa bao moja.
Mpaka anatangaza kustahafu soka hii leo Jason Roberts, amefanikiwa kufunga mabao 137 katika michezo 449 aliyocheza tangu anaanza kucheza soka mwaka 1995, ambapo klabu alizozitumikia ni Hayes, Bristol Rovers, West Brom, Wigan pamoja na Blackburn Rovers.

No comments