Hii ndio nyumba ya Mheshimiwa Temba kapewa na Meneja wake.
Muziki wa Tanzania unazidi kuingia kwenye headline hasa inapotokea kwenye vitu vikubwa kufanyika,mwishoni mwa mwaka jana siku ya Birthday ya Babu Tale,Madee alimkabidhi gari ya kutembelea Meneja wake huyo Babu Talle wa Tip Top Connection.
Kupitia mitandao ya kijamii leo Said Fella Meneja na boss wa Tmk wanaume Family amemkabidhi nyumba Mheshimiwa Temba mjengo ambao uko Kimara Kilungule,na kumbukumbu Temba si msanii wa kwanza kukabidhiwa nyumba na Fella.
Akiongea na 255 ya Clouds Fm Said Fella ameamplify taarifa hizi>>’Nyumba nimemkabidhi mheshimiwa Temba nina utaratibu fulani kwenye uongozi wangu kikubwa nachukuliaga kuwakumbusha vijana hii sanaa sijaianza sasa hivi nimeianza tangu miaka hiyo na vijana wangu wengine niliokuwa nao waka0ondoka’
‘Muziki tuna fanya lakini lazma tuwe na maisha na muono wa baadae kwa sababu leo sauti ipo kesho inachoka lakini tukianza kujiwekeza mapema angalau kuwa vibanda vibanda hivi inaweza kusaidia wakati wowote,ni hela yake mwenyewe namwambia mwanangu tumepata laki moja basi 80,000 weka huku,20,000 kanunue matofali’
‘Kwa sasa kumkabidhi mtu mpaka kuweka kwenye instagram ni mwaka huu lakini nilishamkabidhi Chegge nilishawakabidhi waliotoka sitaki kuwataja kila siku maana wananambiaga kwanini nawataja lakini nishafanya hivi kwa wasanii wangu si chini ya 6 au 7 ‘
‘Thamani yake bado hatujakaa kupiga mahesabu maana ujenzi wake ni wa kimaskini na ufahamu tukipata 100,000 elfu 20 kununua matofali elfu 80 kula na watoto,lakini tukikisikia inafika Milion 20 ina vyumba vitatu vya kulala,ina sehemu ya chakula,parking ya magari ziko mbili tumejenga mpaka sasa Temba na Chegge wana nyumba mbili mbili’.
Hizi ni picha za mjengo huo wa Temba.
No comments