Recent comments

Breaking News

Exclusive:- Avril aeleza kwa nini alimkubali muwekezaji wa Afrika Kusini, adai hakujua ni msanii wakati wako kwenye uhusiano.

Avril aeleza kwa nini alimkubali muwekezaji wa Afrika Kusini, adai hakujua ni msanii wakati wako kwenye uhusiano
Mwanamuziki wa Kenya, Judith Nyambura Mwangi aka Avril ameeleza sababu ya kukubali kuchumbiwa na muwekezaji wa Afrika Kusini na kujitoa moja kwa moja kwenye orodha ya single ladies.
Akiongea kwenye mahojiano na Pulse, mwimbaji huyo wa ‘Chokoza’ amesema mwanaume huyo alimpenda yeye kama Judith Nyambura, msichana wa kawaida na sio msanii wala mtu maarufu kwa kuwa hakufahamu kabisa kama ni muimbaji na muigizaji hadi alipomuona kwenye tamthilia ya ‘Sugar’ kupitia MTV Base, na kwamba wakati huo tayari walikuwa wako kwenye mahusiano.
“Yuko tofauti na wanaume wengine niliowahi kuwa nao kwa sababu yuko ‘interested’ katika kumfahamu na kutoka na Nyambura na sio Avril, mwimbaji.” Alisema Avril.
“Kwa kweli, alikuja kufahamu kuwa mimi ni msanii na muigizaji miezi kadhaa tukiwa kwenye uhusiano wakati anaangalia Shuga, na akaniona.” Aliongeza.  

No comments