D Knob: Baadhi ya wasanii wakongwe hushindwa kufanya vizuri kwa sababu hawako 'flexible', game ina ukungu
Rapper aliyepata mashabiki na kueleweka kwa watanzania wengi kwa mara ya kwanza na wimbo wa Elimu Mitaani, Mr. Sahani aka D Knob ameeleza sababu inayowafanya baadhi ya wasanii wakongwe waliofanya vizuri kwenye game enzi zile kushindwa kufanya vizuri wakati huu.
D Knob ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa kitu kikubwa kinachowafanya wasanii hao wakongwe washindwe kutamba ni kutoweza kubadilika kulingana na nyakati (flexibility).
“Kwa sababu game sasa hivi ina watu wengi kwa hiyo game imekuwa kama ina ukungu hivi. Kwa hiyo wengi wameshindwa kufurukuta kwenye ukungu kwa sababu cha kwanza hawako flexible.” Amesema D Knob.
“Iko ni kitu kikubwa sana kuwa flexible…unajua unapokuwa na watu wengi halafu wote mnataka kula kitu kimoja, ukiwa flexible unaweza ukafyatuka katika njia ambayo wao wanatumia katika kula kile chakula. Ndio maana ya flexibility. Kwamba unaweza njia zote ukaplay ili ufike njia fulani. Wengi hawako flexible.” D Knob amefafanua.
Ameongeza kuwa ili msanii aendelee kudumu kwenye kiwanda cha muziki kwa muda mrefu, lazima mtindo anaotumia uwe na uwezo wa kuishi hata miaka kumi na ukaendana na soko jipya huku akiwa ‘flexible’ pia.
Hivi sasa D-Knob ameanza kufanya miradi ya muziki akiwa tayari ana elimu ya kupanga miradi ‘Project Planning’ ambayo inamsaidia kuendelesha kampuni yake ya Mitaani Most Wanted Ltd.
No comments