Audio: Wakazi aelezea jinsi alivyoupokea wimbo wa Nikki Mbishi unaomchana yeye 'Where my Crown At'
Wiki kadhaa zilizopita Nikki Mbishi aka Terabytes aliachia wimbo alioupa jina la ‘Where my Crown At’, wimbo uliokuwa ukimchana moja kwa moja rapper Wakazi ambaye ndiye aliyeanza kuwasha moto wiki kadhaa zilizopita kwa kumchana rapper huyo kwenye wimbo wake 'ControlVerse'.
Bilingual Beast Wakazi ambaye alikuwa Nigeria kwa muda mrefu baada ya kutoa ControlVerse iliyowachana baadhi ya ma-rapper wa Tanzania huku akiwasifia wengine, alieleza jinsi alivyoyapokea majibu ya wimbo wake toka kwa Nikki Mbishi.
Wakazi alifunguka kupitia The Jump Off ya 100.5 Times Fm wakati akiongea na Jabir Saleh aka Kuvichaka:
“Ujue kitu kama kile inamaanisha kwamba aliguswa na kile nilichokisema. “Unajua mimi nilitoa ControlVerse nilikuwa simlengi mtu mmoja particularly lakini nilimlenga Nikki Mbishi na Godzilla katika line moja moja na wanajua sababu ya mi kufanya vile. Hawawezi kukaa hapa halafu wakasema hawajui sababu ya mimi kuwataja wao…wanajua sababu.” Alisema Wakazi.
“Kwa hiyo mimi nimekutaja kwa mstari mmoja halafu wewe unaniimbia dakika tano. Kwa hiyo inamaanisha kidogo nilichokisema kimekugusa. Na ni ukweli…si unajua ukweli unauma bwana. Ila kiukweli ukweli, let me be clear right now. No body want nothing with me bro.” aliongeza wakazi.
No comments