Recent comments

Breaking News

DR. CHENI: ‘NIMEKUBALI KUOLEWA’ HAISTAHILI KUFUNGIWA…

Uamuzi wa bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuizuia filamu ya muigizaji wa kiume na mkongwe, Dk Cheni ‘Nimekubali Kuolewa’, kwa madai ya kukiuka maadili na kuchochea tabia za ushoga, umepingwa na msanii huyo ambaye anaamini kabisa kuwa maudhui ya filamu hiyo yangeelimisha jamii zaidi ya picha katika cover yake.
Dk Cheni anasema kuwa picha iliyoko kwenye bango la filamu hiyo inayomuonesha akiwa amevaa shera, ndiyo iliyotumiwa na TFB kama kigezo zaidi huku mahudhui yakiwekwa kando.
“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, wamenionea, lengo letu ni kukemea na kupinga vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo kwenye filamu hiyo.” – Dk Cheni.
Msanii huyo alivitaja vipande ambavyo anaamini ilibidi vifikiriwe na TFB kufunika sababu zao zilizopelekea kuzuiwa kwa filamu hiyo.
“Lakini ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvaa shera kwenye cover?” – Dr. Cheni na kusisitiza kuwa uamuzi huo haukuwa sahihi.

No comments