Recent comments

Breaking News

Wasanii kibao wa bongofleva kushirikishwa ndani ya Majanga Remix

Baada ya audio ya Majanga kufanya vizuri hadi kufikia hatua ya kuzaa jina la Team Majanga na hata mwimbaji wa ngoma hiyo kupata jina jipya kwenye gemu ambalo na Mamaa Majanga, Snura Anthony Mushi anatarajia kuja kitofauti zaidi.
“Muziki upo tumeukuta na tutauacha sasa ili wewe ubaki ukikumbukwa lazima ufanye kitu cha tofauti na wenzako lakini kiwe kizuri na hata kama utafanya kitu kilichowahi kufanywa basi inabidi ufanye maboresho ya hali ya juu yatakayomfanya yeyote akubali kwamba wewe upo tofauti ndio maana mimi na meneja wangu huwa tunakaa na kuumiza kichwa sana kuja na vitu tofauti katika gemu. Ujio wangu uliwachangamsha wasanii wengi wa kike kujituma zaidi jukwaani na sasa hivi walio wengi wanatumia kiuno kama silaha yao jukwaani, nikaja na mtindo mpya kabisa kiuimbaji kupitia majanga nayo pia wapo walioufata, sichukii zaidi ya kufurahi kuwa nina kitu ndani yangu. Huu ni mwanzo mengi yanakuja.” – Snura.
Akizungumzia juu ya suala la kushirikisha watu wasanii wengine kwenye ngoma zake au yeye kushiriki kwenye ngoma za watu wengine, Snura alifunguka pia juu ya hilo
“Hadi sasa nimewahi kumshirikisha Wema Sepetu tu kwenye wimbo wangu wa kwanza ‘Shoga yake mama’, lakini baada ya hapo sijamshirikisha mtu ijapokuwa kwenye ile Nimevurugwa ilikuwa mtu mmoja maarufu sana aingize sauti (jina kapuni) lakini sijui ilikuwaje akashindwa kuingiza sauti na kama tungemsubiri basi tungechelewa sana ikabidi itoke vile ilivyo na ikabamba. Sijawahi kushirikishwa ila kama kuna mtu anataka kunishirikisha mimi nipo tayari hata sasa hivi.” – Snura.

Kwa sasa Snura anatamba na kibao chake cha mahadhi ya taarab kiitwacho ‘Uko nyuma sana’, hapa anazungumzia sababu za kutoa kibao hicho na nini kitafuata;
“Hahahaaaaa… Wengi walidhani ngoma itakayofuata ni ‘Ushaharibu’ kwa kuwa tumeitambulisha kwenye mwanzo wa video yangu ya ‘Nimevurugwa’, yawezekana walikuwa sahihi ijapokuwa tuan nyimbo nyingi sana stoo ila na maombi ya fans wangu kuwa nifanye taarab yalikuwa mengi so baada ya kuona kuwa uwezo ninao nikajiuliza kwanini nisifanye hiki kitu pia? na uamuzi ukaja kihivyo na nashukuru imepokelewa vizuri. Pia ni kufanya vitu tofauti kila siku kwa mfano wimbo wa Majanga una Remix yake ambapo humo kuna sauti za wasanii kibao wameshiriki na kila mtu kazungumzia Majanga yake, watu wakae mkao wa kula inakuja ila sijaamua kama ndiyo itakayofuata au niikaushie kwanza.’ – Snura.

No comments