Recent comments

Breaking News

NAVY KENZO KUZINDUA CLOTHING LINE YAO

Navy Kenzo ni kundi muziki linaloundwa na vijana watatu ambao ni Nahreal, Aika na Weaster na halina hata mwaka mmoja tangu lianzishwe na kuanza kufanya kazi rasmi.
Mbali ya kuwa halina muda mrefu sana kwenye gemu la Bongo fleva tayari ni gumzo kutokana na uwezo wao kimuziki katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sababu, nchini Uganda wameshafanya interview na vituo vyote vya nchi hiyo pamoja na kupiga showz nyingikuliko hapa nchini Tanzania.
Kama haitoshi, ndani ya ziara yao hiyo nchini Uganda mwaka jana kati ya mwezi wa tano na sita waliweza kupata promoter ambaye aliwakubali na kuomba kufanya nao kazi kwa upande wa Uganda na kuhakikisha kuwa atazisimamia kazi zao na show zao zote kikamilifu nchini humo.
Mbali na hayo, Navy Kenzo imeweza kushiriki kwenye wimbo wa pamoja unaowakutanisha wasanii kutoka katika nchi tatu uitwao East Africa All Stars, na kwa hapa nyumbani wamechaguliwa wao huku kukiwa na wasanii wengine kutoka Kenya na Uganda.
Hadi sasa Navy Kenzo ina ngoma takriban tano ambazo ni ‘Usinibwage’, ‘Naomba Uniroge’, ‘We do Work’, ‘Kizembe’ na super hit in town kwa sasa ‘Chelewa’. Sifa kubwa inayowatofautisha na makundi mengi hapa Bongo ni pamoja na Kundi hilo kuwa na mavazi yake rasmi ambayo yametokea kuwa kivutio cha wasanii wengine pia. Kutokana na mavazi hayo kupendwa na watu wengi, Navy Kenzo wameamua kuyatambulisha rasmi pamoja na kufungua maduka yao yatakayokuwa yanauza bidhaa zao.
“Haya mavazi nina-design mimi na muda mwingine tunachanganya Idea na crew member wenzangu ili kupata mtindo mzuri zaidi. In short tumekuwa tukipokea order nyingi sana za mavazi yetu kutoka sehemu mbalimbali sasa tumeona ni kwanini tusifanye uzinduzi rasmi na kutoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu bidhaa zetu ili kuwarahisishia watu wasije kuuziwa vitu feki? Ndio maana tukaja na hili wazo sasa.” – Aika
“Tumepanga kufanya uzinduzi huo ndani ya mwezi wa pili mwaka huu na tutazindua mavazi ya kike na ya kiume pamoja na vitu vingine vingi sana bila kusahau utambulisho wa maduka yetu yatakayokuwa sehemu mbalimbali Tanzania. Kwasasa mavazi yetu yanapatikana ndani ya ‘Born 2 Shine’ ile ya B12 ila maduka yetu yanakuja na mtu yeyote atakayehitaji kuwa wakala wa bidhaa zetu popote tunamkaribisha.” – Nahreal.
“Kwa sasa bado hatujaamua kama tutazindulia Arusha au hapa Dar maana sehemu zote hizi kuna watu wanashauri na kushawishi sana tufanyie uzinduzi huko lakini tutakapoamua ni wapi tunafanyia tutatangazana kila Mtanzania atapajua tu.”- Weaster.

No comments