Exclusive:- Je wajua kuwa Sir Alex Ferguson alipewa msimu mmoja kufukuzwa kazi mwaka 1986-1987.
Alexander Chapman Ferguson alizaliwa 31December 1941 huko Glasgow nchini Scotland...Katika maisha yake ya soka amewahi kucheza mechi 317 na kufunga magoli 171 katika nafasi ya ushambuliaji. Mwaka 1974 alianza maisha ya ukocha kwa kuifundisha club ya East Stiilngshire amabapo hakudumu nayo hatimaye miezi kadhaa baadaye alihama na kwenda kuifundisha club ya St. Mirren mnamo mwaka 1974 mpaka 1978. Mwaka 1978 mpaka 1985 alienda kuifundisha club ya Aberdeen baada ya hapo akahamia katika timu ya Scotland ambapoa liifundisha kwa mwaka mmoja. Mwaka 1986 club ya Manchester United ilimuondoa kocha wake
Ron Atkinson ambaye aliichukua club hiyo mwaka 1981-1986 akitokea club ya West Bromwich Albion na baada ya kufukuzwa alirudu tena kwenye club yake ya zamani.
NOTE:- Ameifundisha Manchester United kwa miaka 26 na kuipa jumla ya vikombe 38
Alexander Chapman Ferguson alianza maisha mapya Manchester United mwaka 1986 vibaya baada ya kuwa nafasi ya kumi na moja wakiwa na pointi 56 huku Everton wakichukua ubingwa wakiwa na pointi 86, wakati Manchester City ikiwa ya pili kutoka mwisho na hatimaye kushuka daraja..... Hali hii ilimuweka matatani Sir Alex Ferguson na majarida mabalimbali ya nchi Uingereza yalichapisha habari kwamba Fergie Must go
Msimu uliofuata wa mwaka 1987-1988 Sir. Alex Ferguson alifanikiwa kwa asilimia kubwa baada ya kuipeleka timu yake nafasi ya pili, ambapo walimaliza wakiwa na pointi 81 huku Liverpool ikichukua ubingwa.
Mwaka 1988-1989 mambo yalikuwa mabaya tena baada ya Manchester United kumaliza wakiwa nafasi ya 11 na pointi 51 huku Arsenal wakichukua ushindi wakiwa na point 76. Halii hii haikufanya wamiliki wa club kutaka kumfukuza Fergie ingawa nia yao ilikuwa ni ushindi.
Msimu wa mwaka 1990-1991 Fergie alikuwa kwenye wakati mgumu tena ingawa timu yake ilipanda mpaka nafasi ya sita wakiwa na pointi 60, huku Arsenal ikichukua tena ubingwa wa ligi hiyo. Msimu huu ndio msimu amabo Manchester City ilirudi tena ligi kuu baada ya kushuka kwenye msimu wa mwaka 1985-1986.
Msimu wa mwaka 1992-1993 ndio ulikuwa msimu wa amani kwa Manchester United ambapo ilichukua Ubingwa wakiwa na pointi 82. Fergie alianza maisha ya amani katika club hiyo na kuaminiwa kwa mara ya kwanza na mashabiki wa club hiyo, kwa kuchukua vikombe tofauti kwa mfululizo.
Premier League FA CUP LEAGUE CUP COMMUNITY SHIELD
1993 2007 1990 1992 1990 2003
1994 2008 1994 2006 1993 2007
1996 2009 1996 2009 1994 2008
1997 2011 1999 2010 1996 2010
1999 2013 2004 1997 2011
2000 2013
2001
2003
UEFA CHAMPIONS FIFA CLUB WORLD CUP UEFA SUPER CUP EUROPEANS CUP
1999 2008 1991 1991
2008
No comments