Baada ya Kariakoo na Mbeya sasa Mwanza nao wamegomea mashine za Tra
Suala la machine zinazomilikiwa na Mamalaka ya Mapato Tanzania[Tra]zimeendelea kuwasumbua wafanyabiashara mbalimbali,baada ya 88.5 Kariakoo Dar kugoma na 87.8 Mbeya nao kugomea uwepo wa hizi mashine sasa ni 88.1 Mwanza nao wamegomea hizi mashine
Wafanyabiasha wa maduka ya jijini Mwanza leo wagoma kufungua maduka yao wakigomea mashine za kutolea risiti za EFD toka TRA,maduka mengi mitaa mbalimbali ya Mwanza hayajafunguliwa hizi ni baadhi ya picha za maeneo mbalimbali jijini Mwanza.
Wafanyabiashara walikutana kituo cha zamani cha mabasi cha Tanganyika wakiwa na mabango mbalimbali yanayowasilisha ujumbe wa kupishana na mashine hizo ambapo mbali na makato yake pia kodi nyingine hutozwa pembeni hali wanayoitafsiri kama unyonyaji.
Baada ya Kariakoo na Mbeya sasa Mwanza nao wamegomea mashine za Tra
Reviewed by bongohitz1
on
11:14:00 AM
Rating: 5
No comments