YANGA KULIPIZA KISASI CHA TANO BILA LEO UWANJA WA TAIFA

Ni mtanange wa aina yake wa watani wajadi yaani Simba na Yanga utakaopigwa katika uwanja wa taifa majira ya saa moja jiioni. Simba Sports Club itawakosa wachezaji wake watano mahiri katika safu ya ulinzi, kiungo, winga na ushambuliaji. Japokuwa wapo wengine watakaongoza daraja hilo, huku Young African kujizatiti katika kila sekta kwa kutimia kama kikosi kamili.
Timu hizi zilianzishwa katika miaka ya 1930, ambapo Young Africans ndio ilikuwa timu ya kwanza na pekee kuanzishwa Tanganyika kipindi cha ukoloni, huku Simba ikitokea ubavuni mwa Yanga hivyo kuleta uhasama mkubwa toka kipindi kile mpaka sasa. Ambapo mechi zote wanazokutana kila mmoja anahakikisha kuwa mshindi ili kutimiza dhamira.
Mechi nzima kuoneshwa Super Sport 9EA na TBC1
No comments