BONGO MOVIE KUVUNJIKA KIMYA KIMYA
Mmoja wa wasanii ambao mara zote wamekuwa wakipinga kuwepo kwa klabu hiyo huku ikiendeshwa na wasanii wachache waliojibagua, bila kutaja jina leke, alizungumza na DarTalk na kudai kuwa klabu hiyo imebaki jina kwani kila msanii sasa anajitoa kutokana na lawama hizo zinapelekwa kwao.
Msanii huyo alidai kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao wanaifanya klabu hiyo kama wamezaliwa nayo na hao ndio wamekuwa wa kwanza kujitoa baada gumzo kubwa linaloikabila klabu hiyo huku wakishindwa kueleza uma ni kipi kinachoendelea kutokana na aibu waliyonayo.
“Klabu haipo tena we unadhani kitu kikiendeshwa na watu wanaojiona kama Mungu watu kutakuwa mtu anayeweka mkono zaidi yao na hii ndo umekuwa sababu ya kuvujika kwani kila mtu anajitoa kimya kimya hasemi sababu lakini ishu ni hiyo,” alisema.
Hata hivyp mwandishi alijaribu kuzungumza na wasanii wengine ambao wapo ndani ya klabu hiyo ili nao kujua wana nini cha kuelezea lakini wote walishindwa kusema hali halisi na walibaki kudai kuwa kinachoendelea sasa ni mazungumzo ya kujua klabu inafanya nini kwa lengo la kuiboresha.
No comments