Recent comments

Breaking News

JINSI BEI YA KUPANGA NYUMBA MAREKANI ILIVYOPANDA


New York.
Wakati ambapo mamia ya wabongo wanapeleka maombi ya visa kwenda nchini Marekani, baadhi yao wakiamini kuna urahisi wa maisha.. Shirika la habari la Reuters limetangaza kwamba sasa hivi bei ya kupanga nyumba nchini Marekani imepanda zaidi tangu mwezi march kuanza kwa kiwango ambacho hakijatokea kwa muda miaka kumi nchini humo.
Nyumba ya kawaida imepanda na sasa kwa mwezi ukipanga nyumba yoyote unalipa sio chini ya dola elfu moja na 91 ambayo ni zaidi ya milioni moja ya kitanzania, ambayo ni asilimia moja zaidi ya ilivyokua mwezi wa kwanza mpaka wa tatu mwaka huu likiwa ni ongezeko kubwa tangu mwaka 2007.
Moja kai ya Apartment za Gharama mjini Miami.
Japo gharama za kodi zimepanda kiasi hicho kwa raia wa Marekani, kuna unafuu kidogo kwa sababu serikali ya nchi hiyo inawasaidia kulipa sehemu ya kodi, na wao hawalipi kodi kwa mwaka wala miezi sita, wanalipa kwa mwezi…. Pamoja na hayo, Miji ya New York, Los Angeles na Miami iko kwenye list ya miji inayoongoza kwa kutoza kodi kubwa.
Mfano New York nyumba ya chumba kimoja Manhattan inaweza kufikia mpaka milioni nne za kitanzania kwa mwezi, ni bei ambayo kuna baadhi ya nyumba chache za Masaki Dar es salaam watu wanalipia bei kama hiyo, kwenye dola elfu 3 na kuendelea….
.
Kijitonyama Dar es salaam ambako naambiwa kodi ya chumba kimoja inaanzia elfu 30, 40 mpaka 50.

No comments