HAWA NDIO WACHEZAJI WA SIMBA KOCHA ALIOSEMA HARIDHISHWI NA VIWANGO VYAO.
KOCHA Mkuu wa Simba Milovan Cirkovic amesema kikosi chake hakipo imara katika kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame ambayo timu nyingi zinajiandaa vizuri.
Wachezaji ambao viwango vyao
havijamridhisha ni Haruna Moshi ‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso
na Amir Maftar na hivyo amepanga kuwapa mazoezi kuwarudisha kwenye line.
Simba inatarajiwa kucheza
mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo na URA ya Uganda saa kumi jioni na
mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00 mchana
kwenye Uwanja wa Taifa. (Stori imeandikwa na shaffihdauda.com)
No comments