Haikuishia hapo tu, hata baadhi ya magazeti yalifichua siri kwamba mmiliki wa hiyo nyumba sio Wema ni mama mmoja ambae ni mmiliki wa hospitali moja Dar es salaam.
Lawama za wachache pia zilitolewa kwa Zamaradi Mketema kwamba ameitoa hiyo stori huku akijua sio kweli inamilikiwa na Wema.
Zamaradi ameamplfy na millardayo.com kwa kusema “mimi ni Mwandishi, unapokwenda kufanya interview na mtu ninachotakiwa kusikiliza ni kile ninachoambiwa na mtoa habari lakini sio ninachokijua au kusikia kwa watu, nilimuuliza hii nyumba ni yako? akajibu kweli yeye ndio mmiliki sasa siwezi kubisha, magazeti yanakosea kusema mimi naipotosha jamii ya watanzania… sijaipotosha na kama kweli ile sio nyumba yake mimi sitakiwi kulaumiwa”
Kwenye sentensi nyingine Zamaradi amesema “kwenye show ya Take One ndani ya wiki mbili zijazo Wema amekubali kwamba atautoa uthibitisho kuonyesha kwamba ni mmiliki halali wa hiyo nyumba japo siwezi kuutaja ni uthibitisho gani”
No comments:
Post a Comment