Recent comments

Breaking News

Video: Louis van Gaal atamba kuvuka mafanikio ya Furguson

Meneja wa klabu ya Man utd Aloysius Paulus Maria van Gaal, amepasua ukweli wa kukubali kujiunga na klabu hiyo ya mjini Manchester kwa kusema ukubwa na mafanikio yaliopo huko Old Trafford ndicho kilichomsukuma kufanya kazi chini ya mashetani wekundu.
Van Gaal aliye nchini Marekani kwa sasa sambamba na kikosi chake kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu wa mwaka 2014-15, amesema alikua amepata ofa kutoka kwenye klabu kadhaa lakini alipima na kuona Man Utd inamfaa.
Amesema amewahi kufanya kazi nchini kwao Uholanzi, akiwa na klabu kubwa ya Ajax Amsterdam, kisha akafanya kazi na klabu ya Barcelona na baadae aliekelea nchini Ujerumani kuitumikia klabu yenye mafanikio Fc Bayern Munich hivyo aliona kuna umuhimu wa kuendeleza wasifu wake kwa kuwa muajiriwa wa Man Utd.
Wakati huo huo Louis Van Gaal ametoa angalizo kwa mashabiki wa klabu ya Man utd ulimwenguni kote kwa kuwaambia wasiwe na pupa ya kupata mafanikio na kuamini kuelekea kwake Old Trafford huenda kukaleta mabadiliko ya haraka.
Amesema kila shabiki wa klabu hiyo anachotakiwa kufahamu kwa sasa van Gaal ni binaadamu kama alivyo yeye, hivyo anaweza kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa wakati huu na pengine wakati ujao.

No comments