Picha za Staa wa Barcelona alieoa zimeshatoka tayari, ziko hapa.. chek pia Messi, Fabregas na wengine walivyotokelezea na wake zao yani
Jumapili July 14 2013 ilikuwa siku ya furaha kwa staa wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Xavi Hernandez ambapo alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Nuria Cunnillera, ni harusi iliyofanyika huko Catalunya kanisani kabla ya hafla ya aina yake iliyofanyika kwenye bustani maarufu za Marimurta kaskazini mwa jimbo la Catalunya ambapo wageni 180 walihudhuria wakiwemo mastar wengi wa Barca, timu ya taifa ya Hispania na wengine.
Mke wa Xavi Nuria ni mtangazaji wa vipindi vya mitindo kwenye televisheni nchini Hispania na kwa sasa wawili hao wamekuja kula honey moon yao barani Afrika kwenye visiwa vya Shelisheli (Seychelles).
No comments