Recent comments

Breaking News

JOYCE KIRIA PRESENTS MSIMU MPYA WA WANAWAKE LIVE.

Wanawake live ni kipindi kinacho rushwa na EAtv na Magic Swahili kwa siku tofauti tofauti za juma na lengo kubwa ni kuwapa fursa wanawake pamoja na kuziangazia malengo yao.
Joyce Kiria ni miongoni mwa wa watangazaji wenye uthubutu wa kufanya kitu kwa kuwakomboa wanawake na wasichana wasio na sauti katika jamii kupitia kipindi chake cha wanawake Live.
Kutokana umaridadi wa Joyce Kiria alias staring wa Wanawake Live amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kuwafikia wanawake wa mjini na vijijini kwa kuongea nao kuhusiana na mwenendo mzima wa maendeleo katika maisha.

Msimu mpya wa Joyce Kiria katika kipindi cha Wanawake Live ni ujio uliobeba mahudhui makubwa ya kumkomboa mwanamke kiuchumi, kisiasa pamoja na kijamii ili aweze kusonga mbele kimaendeleo.

Staring wa Wanawake Live alitembelea Mkoa wa Dodoma, Pwani na vijiji vyake kwa lengo la kuwafikia wanawake waliopo vijijini humo ili kujionea fursa zao na kujua changamoto wanazokabiliana nazo.
Kaa mkao wa kuangalia msimu mpya katika luninga yako ya EAtv na Swahili Magic

No comments