HUU NDIO WOSIA WA LADY JAY DEE IKITOKEA KIFO CHAKE

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila
nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na
mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo
mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii
industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni
kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa
inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi
yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
No comments