MAMA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA ATOA FILAMU MPYA INAYOITWA "WITHOUT DADY"

MAMA Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba’ Frola Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye baada ya kuigiza katika filamu ya Without Daddyakishirikiana na watoto waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na Jamila, katika filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.

Ben Blanco akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.

Mama Kanumba mwigizaji.
Filamu ya Without Daddy imeshirikisha wasanii nyota wengi kama vile Abdalah Mkumbilah ‘Muhogo mchungu’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ Cathy Rupia, Mayasa Mrisho, ‘Maya’, Othuman Njaidi ‘Patrick’ Wastara Juma ‘Stara’ Abdul Ahmed ‘Ben Blanco’ na wasanii mahiri wengineo.
No comments