CHELSEA HII STORI DIZAINI KAMA INAWAHUSU INAMUHUSU MKALI WENU ASHLEY COLE.
Kupitia vyombo mbalimbali vya habari vinavyotoa michapo ya michezo kila siku nchini U.K vimeipa stori ya Ashley kichwa cha habari “Chelsea wanaweza kumuuza Cole January mwakani”
PSG ya Ufaransa iliyopanga kumnunua mchezaji huyu staa wa Chelsea, unaambiwa zipo club nyingine kubwa kwenye list ambazo ni Real Madrid, Man U na Man City ambazo ziko tayari kutoa poundi laki moja na nusu kila wiki na mkataba wa miaka mitatu unaoaminika kuwa na thamani ya pound milioni 23.
Baada ya Ashley Cole kushindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na Chelsea, club tajiri ulaya ikiwemo PSG zimetangaza nia ya kumsajili staa huyu mwenye umri wa miaka 31.
Kama Ashley Cole na Lampard wataondoka Chelsea, wataalamu wa mambo wanasema timu hii iliyochukua ubingwa wa Ulaya itakua imesambaratika japo inasemekana kwamba mmiliki wake amepanga kuhakikisha hivyo vichwa haviondoki, tofauti na tetesi zilizo kwenye vyombo vya habari.

No comments