BREAKING NEWS:- VURUGU ZA MBAGALA ZAHAMIA MJINI, WAISLAMU WAANDAMANA NA KUZINGILA KITUO CHA POLISI
Habari
zilizotufia hivi punde kutoka katika chanzo cetu cha habari ni kwamba kuna vurugu
zinazoendelea sasa maeneo ya mjini, stesheni katika kituo cha polisi, ambapo
waislamu wameandamana na kukizingila kabisa kituo hicho cha polisi na kutaka
kuachiwa kwa Sheikh wao, hii ni baada ya kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda (Katibu wa taasisi za jumuiya ya Kiislamu) aliyekuwa
akiitaka polisi iwaachie waislam waliokamatwa katika vurugu za Mbagala baada ya
kuchoma makanisa kadhaa huko Zakiem. Mpaka sasa maduka yote ya wafanyabiashara
huko mjini yamefungwa na hakuna huduma au shughuli yoyote inayoendelea kwa
sasa.
Polisi
wamedhibiti katika mitaa kwa kutumia mabomu ya machozi na magari yanayotoa maji
yenye kuwasha katika hali ya kuleta amani na kutaka kuwatanya waandamaji hao
kwa kutuliza ghasia, mpaka serikali itakapotia shauri lake juu
ya suala hili, ili amani iwepo.
 
Tutaendelea
kuwajuza yatakayojiri.

Mmoja
 wa wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye imani kali akidhibitiwa na 
polisi mara baada ya kukamatwa leo katika kituo kikuu cha polisi Kati 
wakijaribu kuandamana ili kushinikiza kiongozi wao Katibu wa Taasisi za 
Kiislamu Shekh Ponda Issa Ponda kuachiwa na jeshi la polisi mara baada 
ya kukamatwa jijini Dar es salaam kwa kudaiwa kusababisha vurugujijini 
Dar es salaam.

No comments