HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA MAPACHA WATATU BAADA YA KUACHANA RASMI NA KALALA JUNIOUR..
Exclusive ni
kwamba Josee Mara ambae ni kiongozi na mmiliki wa band ya MAPACHA
WATATU amesema “Kalalaaliyekua mkurugenzi wa Mapacha tumeshaachana nae
mazima kwa sababu ilikua ni mjadala wa mda mrefu, Tumeshamalizana nae na
zile taratibu alizoziomba zimeshafanikiwa na tumeshafanya mikataba
chini ya Advocate Okale”
“Kikubwa sasa hivi tunaangalia
tunafanya nini ili kuwapa nafasi wanamuziki tulio nao MAPACHA akiwemo
Catherine, January na Kambi… yani kama Josee Mara aliimba rangi ya
chunga na Jojina ndani ya FM ACADEMIA miaka miwili na ndio akaja kutoka
kwenye dunia kigeugeu basi mi naamini January na Kambi tutawapa nafasi
na maisha yataendelea” – Josee Mara
KUHUSU KUBADILI JINA BAADA YA
PACHA WATATU KUONDOKA:
“Hatuwezi kubadili jina kwa sababu ni Brand huyo
watatu atakua ni msikilizaji na mtazamaji ambae atakua anaisupport
Mapacha” – Josee MaraJosee Mara mtoto wa Kimara amekanusha stori kwamba chanzo cha kuondoka kwa Kalala ni ugomvi uliotokea kati yao wawili, mbali na kukanusha akaongeza kwamba “hizo ni fununu tu na sijawahi kugombana nae na ndio maana leo wanasema ni Kiso kesho wanasema ni Jose basi waangalie na kesho kutwa wasije kusema ni Millard Ayo”
Kalala Junior ambae wiki mbili zilizopita kupitia millardayo.com alitangaza kwamba amesimama kufanya muziki kwa muda wa miezi miwili amefanya kazi na Mapacha watatu kwa miaka miwili ambapo taarifa za yeye kuacha kufanya kazi na band hiyo alizitoa kwa wenzake mwezi mmoja uliopita baada ya kumaliza kufanya moja kati ya show zao za usiku.
Kwenye hii album mpya ya Mapacha haitosikika sauti ya Kalala na pia hata kwenye single mpya waliyofanya Mapacha na kumshirikisha Ally Kiba, sauti ya Kalala haijasikika…….. na hiyo haimaanishi chochote kwamba Kalala na wenzake hawako kwenye uhusiano mzuri, bado wanaongea lakini kikazi ndio hawako pamoja.
Kwa kumalizi, Josee Mara amesema siku zote unapozoea kukaa na mtu akiondoka lazima ujisikie huzuni lakini baada ya muda flani unasahau, hicho ndio kinachotokea kwa Mapacha sasa hivi baada ya Kalala kuondoka lakini haijawaathiri kwa njia yoyote ile kwenye uchumi wa band yao, bado wanaendelea kupokea vichwa kama kawa.
No comments