PICHA ZA AJALI YA HELCOPTER ILIYOUA MAWAZIRI KENYA LEO.
Imethibitishwa kuwa Waziri wa 
usalama wa taifa wa Kenya Profesa George Saitoti pamoja na msaidizi wake
 Joshua Ojode ni miongoni mwa watu saba waliofariki dunia kwenye ajali 
ya helicopter ya Polisi iliyotokea kati ya saa tatu au saa tano leo 
asubuhi huko Ngong Kenya.
Citizen Tv wameripoti kwamba 
inaaminika chanzo cha ajali ni kutokana na hali mbaya ya hewa ambapo 
helicopter hiyo ilikua na marubani wawili akiwemo mmoja wa kike.
Kifo hiki kinaingia kwenye 
kumbukumbu ndefu ya wakenya kwa sababu tarehe kama ya leo miaka minne 
iliyopita helicopter nyingine ya Polisi ilipata ajali na kuua mawaziri 
wawili wa Kenya.



















No comments