IJUE TANZANIA YAKO NCHI YENYE UDONGO WENYE DHAMBI
Natumaini sote
ni wazima katika harakati za ujenzi wa taifa letu, ambapo wanasiasa wachache
wanaoficha maovu yao
nyuma ya mazabao wanaliita ni taifa changa. Kwa mtazamo wangu Tanzania si taifa
changa bali Tanzania ni taifa lilofunikwa na udongo wenye dhambi.Dhambi ambazo
zinatesa wale wasiokuwa nacho kuwa chini ya waliokuwa navyo na kuwa watumwa
ndani ya nchi yao.Hii ni dhambi ambayo inahitaji makemeo ya hali na mali ili
kupisha uongozi safi.
Ikumbukwe kuwa Desemba
09’1961 Tanzania
ilipata uhuru wake kutoka kwa Muingereza, ambaye alikuwa mtawala baada ya
ukoloni wa Ujerumani. Ambapo Hayati Mwl.julius K.Nyerere ndiye aliyetawazwa
kuiongoza Tanganyika kama waziri mkuu mpaka mwaka 1962 ambapo
ndipo Tanganyika
ilipata Jamhuri na kuwa na raisi wake. Toka mwaka 1961 mpaka miaka ya 1970 Tanganyika
ilikuwa inatumia katiba iliyoachwa na muingereza. Lakini mwazoni mwa miaka ya
1970 Tanganyika baada ya
kuungana na Zanzibar
mwaka 1964, ilisahihisha na kurekebisha pasipo kubadilisha katiba hiyo.
Japokuwa inasemekana kwamba ilibadilishwa kwa mitazamo isiyo wazi. Hii ina
maana ya kwamba haikujali Demokrasia ya kweli kwa raia wake, Lakini hakuwepo
mtetezi wala aliyedhani juu ya hili.
Vuguvugu la
uongozi bora juu ya kuwakandamiza wahujumu uchumi liliendelea wazi serikalini
katika uongozi wa awamu ya kwanza. Hii ilipelekea Hayati Mwl.Julius K. Nyerere
kuleta azimio la Arusha mnamo mwaka 1967. Ambapo azimio hilo lilikuwa
likitetea sera ya uongozi bora,ambapo Mwalimu alikemea baadhi ya mambo ili
kufanya Tanzania
kuwa na tija katika uchumi wake. Hii ilikuwa ni kuhakikisha kuw hakuna
atakayethubutu kufanya uhujumu uchumi katika serikali yake. Na pia kuhimiza
baadhi ya mambo katika serikali yake ikiwemo siasa ya ujamaa.
Lakini Azimio
halikudumu, lilikandamizwa na kupigwa chini na wajanja wachache ambao
walihitaji kujinufahisha. Tanzania
haikufahulu katika hilo
hivyo kufanya raia wake kubaki masikini na kuzidi kuwa wanyonge ndani ya taifa
huru bandia.
Mwaka 1992,
Mwalimu alileta hoja ya mfumo wa vyama vingi, ambapo kura za maoni zilipopigwa
Watanzania baadhi hawakutaka mfumo huu, lakini Mwalimu akataka mfumo huo upitishwe
na mchakato wa usajili wa vyama vya siasa uanze mara moja.Wapo ambao wanasema
kwamba hii ilikuwa ni hekima ya Mwalimu,lakini wachunguzi na wataalam wa siasa
wanadai kwamba hii ilitokana na nchi zilizoendelea huko ulaya pamoja na benki
ya dunia kutaka nchi zote za Afrika ziwe ndani ya mfumo wa vyama vingi ili
kupisha demokrasia ya kweli kwa nchi hizo.
No comments